Alhamisi 18 Septemba 2025 - 22:43
Mauaji ya Kimbari ya Wapalestina ni Matokeo ya Utendaji wa Ukoloni Duniani

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Seyyed Sajid Ali Naqvi, Raisi wa Baraza la Waislamu wa Kishia nchini Pakistan, katika tamko lake alieleza kwamba; Israel ni zana tu ya ukoloni wa dunia, na kwamba ukoloni wa dunia ndio chanzo kikuu cha mauaji ya kimbari ya Wapalestina, na alieleza kuwa “Muqawama” ndii ishara ya matumaini Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Raisi Naqvi, akionesha wasiwasi wake kuhusiana na mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel katika mji wa Ghaza na kuhamishwa kwa lazima Wapalestina kutoka ardhi kwenye zao, alisema: “Sasa kila kitu kimekuwa wazi, Israel ni zana tu, na muuwaji wa asili mauwaji ya kimbari, njaa na ukatili usio wa kibinadamu huko Ghaza ni ukoloni wa dunia.”

Aliongeza kusema huku akirejelea “Muqawama”, kuwa harakati hii ya msaada ni ishara ya matumaini na mwanga katika hali ya giza na ukombozi wa Ghaza, na akaongeza kusema: “Muqawams ni kama taa inayong’aa katikati ya giza la hofu na ukatili.

Raisi wa Baraza la Waislamu wa Kishia nchini Pakistan aliendelea kusema: “Baada ya mashambulio ya Israel dhidi ya Qatar, ilitarajiwa kwamba mkutano wa viongozi wa Kiislamu ungechukua hatua za ujasiri na zenye matokeo madhubuti kuhitimisha dhuluma na ukatili dhidi ya Wapalestina, na kurejesha sehemu ya heshima iliyopotea ya Ummah ya Kiislamu, hata hivyo, kwa bahati mbaya, tamko lililotolewa, hata kabla ya wino kukauka, lilifuatiwa na ukatili mwengine kutoka Israel ambao, kwa msaada wa zile nguvu za dunia, iliendelea na mauaji ya kimbari na dhuluma zake.”

Aliongeza kusema: “Sasa imebainika wazi kwamba Israel ni zana tu, na chanzo kikuu cha mauaji ya kimbari, njaa na dhuluma dhidi ya ubinadamu ni ukoloni wa dunia, ambao hata baada ya kuuawa kwa maelfu ya watu, unaendelea na uhalifu wake.”

Raisi wa Baraza la Waislamu wa Kishia nchini Pakistan alizungumzia pia “Meli za Muqawama”: “Kikundi hiki cha msaada, kinachojumuisha takriban meli 70 na mashua ndogo zenye wawakilishi wa haki za binadamu kutoka nchi 44, na kuondoka kutoka Hispania tarehe 31 Agosti, ni ishara ya mwanga wa matumaini katikati ya giza la ukatili na ujumbe wa ubinadamu katika hali ya vurugu za leo.”

Alimalizia kwa kusisitiza: “Ingawa msaada huu hauwezi kuondoa mateso ya waliodhulumiwa kikamilifu, unaweza kuwa kama tone la kwanza la mvua ya rehema na matumaini, ni muhimu kwamba jamii ya kimataifa na dunia ya Kiislamu zipewe rasilimali zote, usaidizi na usalama unaohitajika ili kikundi hiki cha meli kifikie mahali panapohitajika, na hivyo kupunguza maumivu ya walio dhulumiwa.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha